Jumamosi 25 Julai 2026 - 20:43
Tunaunga mkono hatua za Yemen za kumaliza mzingiro wa kidhalimu na kutoa jibu la kulipiza kwa msingi wa haki

Hawza/ Kikao cha vyama, makundi na shakhsia za kitaifa za Lebanon kimesisitiza mshikamano wake na haki ya wananchi wa Yemen ya kumaliza mzingiro wa kidhalimu uliowekwa dhidi yao, pamoja na haki yao ya kutoa jibu la kulipiza ili kukomesha dhulma wanazofanyiwa.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kikao cha vyama, makundi na shakhsia za kitaifa za Lebanon, huku kikilaani kuendelea kwa mzingiro uliowekwa dhidi ya wananchi wa Yemen ambao umebeba mzigo mkubwa kwa raia na kuongeza mara dufu mateso yao ya kibinadamu na kiuchumi katika nyanja mbalimbali, kimesisitiza mshikamano wake na haki ya wananchi wa Yemen ya kumaliza mzingiro huo wa kidhalimu ambao wamewekewa kwa miaka mingi, pamoja na haki yao ya kujibu kwa hatua za kulipiza ili kukomesha dhulma wanazofanyiwa.

Katika taarifa yake, kikao hicho kilisema: "Katika mazingira ya kuendelea kwa mateso makubwa ya kibinadamu yanayowakumba wananchi wa Yemen kutokana na mzingiro wa kidhalimu dhidi ya bandari na viwanja vyao vya ndege, huku pande nyingine zikiendelea kung'ang'ania misimamo yao na kukataa kujibu madai ya haki na ya kibinadamu ya wananchi wa Yemen, ni haki ya msingi ya wananchi wa Yemen kutetea heshima yao na kutumia njia zote halali ili kuondoa dhulma wanazofanyiwa."

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa; kuondolewa kwa mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen, kushughulikiwa kwa suala la mishahara na masuala mengine ya kibinadamu, pamoja na kuwawezesha Wayemeni kusimamia na kutumia utajiri wao wa kitaifa, ni haki za kibinadamu na za kitaifa ambazo hazipaswi kuwa sehemu ya mazungumzo au maridhiano ya aina yoyote.

Kikao hicho pia kilitangaza kuwa kinaunga mkono hatua na mikakati ya kujihami ya kisheria inayochukuliwa na Serikali ya Sana'a katika kujibu mzingiro huo kwa hatua za mzingiro wa kulipiza, kwa kuwa hatua hiyo ni nyenzo ya dharura iliyolazimishwa na haja ya kuondoa dhulma na kuvunja mzingiro uliowekwa dhidi ya maisha na uchumi wa wananchi wa Yemen.

Taarifa hiyo iliendelea kusema: "Ni haki ya wananchi wa Yemen kuchukua hatua za kuongeza shinikizo kwa utaratibu na kwa umakini dhidi ya serikali ambazo zinaendelea kung'ang'ania mzingiro huo. Hatua hizo zinalenga kuweka shinikizo kwa bandari na rasilimali za nchi hizo ili kuzilazimisha kujibu madai halali ya Yemen bila masharti yoyote."

Mwishoni mwa taarifa hiyo, vyama vya Lebanon vilieleza kuwa; bado kuna fursa kwa serikali zinazohusika na mzingiro huo kuzuia athari kubwa za kiuchumi na kibinadamu. Hilo linawezekana kwa kuanza mara moja kuondoa kikamilifu mzingiro dhidi ya bandari zote na viwanja vyote vya ndege vya Yemen, kushughulikia masuala ya dharura ya kibinadamu — likiwemo suala la kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakati — kuheshimu mamlaka na uhuru wa Yemen, pamoja na kuwawezesha wananchi wa Yemen kutumia utajiri wao kwa ajili ya maendeleo na uthabiti wa nchi yao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha